About HAYATE ORGANIC FARMS
Hayate Organic Farms kampuni ya inayojishughulisha na kilimo cha mazao mbali mbali, kutoa huduma za usimamizi wa mashamba,kusafisha mapori ya wateja pamoja kuwapandia mazao wanayohitaji pamoja na kutoa huduma hizo pia tunatoa ushauri kwa watu wanaotarajia kuingia kwenye kilimo.
Mission
Hayate organic farms tunashughulika na kilimo cha matunda ya strawberry,blackberry na raspberry pamoja na miche yake kwa mkoa wa Mtwara tunalima zao la Korosho pamoja na miche yake pia tunauza korosho nyeupe za kula, kwa mkoa wa Tanga tunalima zao la Katani ( Mkonge) wilaya Handeni vijijini pamoja na kuuza miche yake bora pia kwa mkoa wa Pwani bagamoyo na Pangani tunalima zao la Nazi pamoja na kuzalisha miche yake bora kabisa mbegu aina ya Pangani one Hayate Organic Farms tunazalisha miche ya Karafuu,Hiriki,Mdarasini,miti ya mbao aina ya mitiki. Sambamba na hivyo tunatoa semina ya elimu kwa wakulima mbali mbali juu matumizi sahihi ya mbolea mashambani kwenye mazao yao, matumizi sahihi ya viwatilifu vyakuangamiza wadudu wahalibifu wa mazao,magonjwa ya mimea na jins yakuandaa shamba kwa ajili ya kilimo tunahakikisha tunawafikia kila kundi kila taasisi ya kidini shule mbali mbali elimu hii tunatoa bure ila kwa gharama za kuhudumia nauli,chakula na makazi kwa sehemu zinazohitaji huduma hizo kwa mkufunzi.
Vision
Hayate Organic Farms malengo ni kuhakikisha ifikapo 2025 tuwe tumeweza kuzalisha nazi kwa ukubwa wa Hekta 250 na kuanzisha kiwanda cha kukamua Mafuta ya Nazi kwa matumizi ya kula na kujipaka lkn pia sambasamba na hivyo tuna malengo yakutanua wigo mpana kwakuongeza mashamba makubwa kwa mkoa wa Tanga kwa ajili yakuzalisha zao la Katani ili tuwe msambazaji mkubwa ndani nje ya nchi. Lakini pia nikuhakikisha tunatoa ajira kwa wanawake na vijana ili kuhakikisha na wao wanajiongezea kipato na kuendesha Maisha yao na familia. Malengo yetu ifikapo 2025 tuwe tumeweza hamasisha vijana Zaidi ya 500 kujiajiri kwenye kilimo kwakuwapa elimu bure kwenye mashamba yetu huku wakipatiwa chakula na malazi bure kisha kujiunga kwa vikundi vya watu 5 kisha kuwaombea mkopo wa 10% unaotengwa na halmashauri ya wilaya ambao hauna riba